Thursday 3 July 2014

MAJAMBAZI WASHAMBULIA GARI LA MAGEREZA KWA RISASI DAR-SOMA STORI KAMILI

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
                                                                         2

SHUHUDA

Ishu ilikuwa hivi, kuna gari ndogo ilikuwa inatokea njia ya Kawe kwenda Shopperz au ilikuwa inaelekea mjini kwa kutumia hii njia ya Mwai Kibaki road.

Hiyo gari ndogo ilipofika Maeneo ya Million Hairs Salon jirani kabisa na Regency park hotel ikakwama kwenye foleni ndefu sana. Nyuma ya hiyo gari ndogo kulikuwa na magari mengine yameunga hiyo foleni.
Gari ya magereza ikiwa na wafungwa ilikuwa ni kama ya sita au ya nne nyuma ya hiyo gari ndogo mara ghafla tukasikia puuu! puuu! pooo! poooo! poooo!  kama risasi 6 au 8 hivi – kumbe ile gari ndogo inavyosemekana ilikuwa imebeba kiasi kikubwa cha pesa na hakukuwa na escort yoyote. 

Majambazi wakiwa kwenye pikipiki waliifuata ile gari pale kwenye foleni wakamuamrisha yule jamaa atoe fedha na jamaa akaachia mkwanja.
 1
Sasa lile gari la magereza kwa vile liko juu sana kama gorofa askari wake wakaiona hiyo ishu live. Sasa ile wanajiandaa tu na mabunduki yao majambazi nayo wakashitukia mchezo na wakaanza wao kuwashambulia kwa risasi wale askari magereza.

Askari magereza ile wanajiandaa kujibu mapigo tu majambazi haooooo wakawasha pikipiki na kuondoka kwaspeed ya 220.
432
Kiukweli ilitisha na watu waoga kama mimi nilikimbilia kujificha sehemu. Yaani ilikuwa kama Movie
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger