Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesema Tanzania kwa sasa
ina hazina ya kutosha ya makaa ya mawe na gesi itakayowawezesha
wawekezaji kupata nishati ya uhakika.
Waziri
Muhongo pia ameahidi kuendeleza mradi wa usambazaji umeme vijijini ili
kutimiza lengo la kila mtanzania kuwa na uhakika wa kupata nishati ya
umeme.
Profesa
Muhongo amesema hayo jana Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa
kikanda wa masuala ya nishati endelevu uliwakutanisha washiriki kutoka
nchi kadhaa ndani na nje ya bara la Afrika.
Katika
mkutano huo, Waziri Muhongo aliwataka wadau hao kutafuta suluhisho la
upungufu wa nishati kwa kuzingatia malengo ya milenia yanayotaja nishati
kama moja ya sababu za kuinua uchumi.
Kwa
upande wake, Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alvaro
Rodriguez alisema nchi za Afrika zinahitaji kutumia teknolojia, sera na
uwezo walio nao katika kupambana na suala la upungufu wa nishati huku
umoja huo ukiahidi kutumia jumla ya dola za Kimarekani bilioni mbili
katika kuwezesha upatikanaji wa nishati endelevu.
0 comments:
Post a Comment