Siku chache baada ya Rais Dokta John Pombe Magufuli kuwataka wakuu wa
mikoa na wakuu wa wilaya zote nchini kuacha kuwabughudhi wamachinga na
badala yake wawatafutie maeneo maalumu ya kufanyia biashara zao hali
imekuwa tofauti kwa Manispaa ya Morogoro baada ya wafanyabiashara
mbalimbali kuyatelekeza masoko na kupeleka bidhaa zao katikati ya mji
huku wafanyabiashara wa maduka wakilalamikia maduka yao kuzibwa na
bidhaa hizo.
Wakizungumza na ITV wafanyabiashara hao wa maduka wametupia lawama
uongozi wa wilaya kushindwa kusimamia agizo la Rais kwani
wafanyabiashara wanaosambaza bidhaa chini na kuziba maduka sio wale
aliowalenga Mheshimiwa Rais Magufuli.
ITV imeshuhudia meza na vikazi vikiwa wazi katika soko kuu la Manispaa
la Manzese walikohamishiwa wafanyabiashara wote huku waliobaki nao
wakiazimia kulitelekeza soko hilo na kufuata wateja maeneo ya
mjinikushinikiza waliotoroka kurejeshwa sokoni hapo.
Kufuatia malalamiko hayo mkuu wa wilaya Morogoro Bi.Regina Chonjo
amesema serikali haitawavumilia wafanyabiashara walionukuu vibaya kauli
ya Rais na badala yake halmashauri inapanga utaratibu wa kuhakikisha
wale wote waliotoroka katika maeneo yao ya biashara na kuwa kero kwa
wengine wanarudishwa mara moja.
chanzo: Itv
0 comments:
Post a Comment