Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF) limesema kuwa mechi ya ligi kuu Tanzania Bara ya
mzunguko wa pili kati ya Simba na Yanga iliyokuwa imepangwa kuchezwa
Februari 18 mwaka 2017 iko palepale kwa kuwa bado halijafikiria
kuibadili tarehe hiyo.
Hatua
hiyo inatokana na tarehe hiyo kugongana na kalenda ya CAF ya michuano
ya Klabu Bingwa Barani Afrika iliyotolewa hivi karibuni na kuipanga
Yanga kucheza mchezo wa marudiano kati yake na Ngaya de Mbe ya Comoro
kati ya tarehe 17, 18 na 19 mwezi Februari 2017.
Afisa
Habari wa TFF Alfred Lucas amesema kuwa hadi sasa shirikisho hilo
kupitia Bodi ya Ligi halijafikiria kufanya mabadiliko yoyote kwenye
ratiba hiyo, na kwamba ratiba itaendelea kubaki kama ilivyo hadi hapo
itakapotangazwa vinginevyo.
"Ratiba
imeshapangwa na haitabadilika, kila timu inajua itacheza lini, kuhusu
ratiba ya CAF haiwezi kutuzuia kufanya mashindano yetu, kama kuna timu
inacheza CAF inatakiwa ijipange, kila timu inatakiwa kuwa tayari wakati
wowote ndiyo maana zinafanya matayarisho, zinaajiri makocha, zinasajili
wachezaji , hiyo yote ni matayarisho kwahiyo sidhani kama watahitaji
kupumzika na kutuharibia ratiba" Amesema Lucas
Jumatatu
iliyopita Mtendaji Mkuu wa Bodi ya ligi Boniface Wambura akiwa kwenye
kipindi cha 5Sports cha EATV, alisisitiza kuwa katika mzunguko wa pili
wa ligi, ratiba haitakuwa tatizo, na kwamba haitabadilishwa badilishwa
kwa kuwa katika upangaji wake kila kitu kilizingatiwa ikiwemo kalenda ya
CAF.
0 comments:
Post a Comment