Kwa
hali isiyo ya kawaida sungusungu zaidi ya mia nane wamevamia kijiji cha
Welezo katika kata ya Tinde wilayani Shinyanga na kutembeza kichapo kwa
wakazi wa kijiji hicho hali ambayo imezua taharuki na kusababisha
kamati ya ulinzi na usalama ikiongozwa na mkuu wa wilaya hiyo kuingilia
kati na kumsimamisha kazi mwenyekiti wa kijiji hicho kwa kosa la kufanya
uzembe uliosababisha vurugu.
Mwandishi wetu amefika katika kijiji hicho cha Mwelezo na kukuta baadhi
ya wananchi waliopata kipigo wakimlalamikia kamanda wa sungusungu wa
wilaya ya Shinyanga kualika kundi la watu na kuamrisha yasomwe majina ya
baadi ya watu kwa madai kuwa ni wahalifu na kuadhibiwa kwa kuchapwa
viboko kosa ambalo wamedai limetokana na wao kudai kusomewa mapato na
matumizi katika mikutano ya kijiji kwa muda mrefu bila mafanikio.
Akitoa kauli ya kumsimamisha kazi mwenyekiti wa kijiji cha Welezo
bw.Salum Shabani mkuu wa wilaya ya Shinyanga Bi.josephine Matiro amesema
amelazimika kuunda uongozi mpya wa jeshi la sungusungu pamoja na
kumteua Bi.Janeth Kurubone kukaimu nafasi ya uenyekiti hali ambayo
imemlazimu mwenyekiti huyo aliyesimamishwa kuondoka katika mkutano huo
mara moja kwa hofu ya kupigwa na wananchi waenye hasira kali.
Kulwa Masanja ni Kamanda wa sungusungu wa wilaya ya Shinyanga
anayetuhumiwa kualika kundi la sungusungu zaidi ya 800 kuwaadhibu
wananchi wa kijiji hicho cha welezo amelazimika kuomba msamaha na kudai
kuwa alichomekwa bila kujua huku mbunge viti maalum wilaya ya Shinyanga
Mh.Aza Hilali akikiri kuwepo kwa migogoro ya muda mrefu inayosababishwa
na baadhi ya viongozi wa serikali ngazi ya kata vijiji na vitongoji
kutokuwa waaminifu kwa wananchi.
Chanzo: itv
0 comments:
Post a Comment