Mwanafunzi wa kidato cha pili wa shule ya sekondari Mringa, Vanessa
Josephat [16] mkazi wa Sakina jijini Arusha amejeruhiwa vibaya kwa
kupigwa risasi kichwani na walinzi wa kampuni ya ulinzi ya kifaru
waliokuwa wakiwatoa kwa nguvu kwenye nyumba yao yenye mgogoro .
Tukio hilo limethibitishwa na kamanda wa jeshi la polisi mkoani Arusha
Charles Mkumbo ambaye alisema kuwa polisi inamshikilia Fabian Charles
mlinzi wa kampuni ya kifaru pamoja na silaha aina ya shoot gun iliyo
tumika katika tukio hilo huku majeruhi amelazwa katika hospitali ya KCMC
kutokana na hali yake kuwa mbaya .
Kamanda mkumbo alisema kuwa tukio hilo limetokea jana majira ya saa tatu
asubuhi katika eneo la sakina jijini hapa, ambapo alisema walinzi
watatu wa kampuni hiyo waliokuwa wakilinda nyumba hiyo inayomilikiwa na
Josephat Nehemia walitumia silaha hiyo kuwafyatulia familia inayoishi
hapo ili waondoke na ndipo silaha hiyo ilipomjeruhi mwanafunzi huyo .
Taarifa zinaeleza kuwa December 21 mwaka huu kampuni ya udalali ya Marc
Recorders Limited wakiwa na mabaunsa na watu wengine walivamia nyumba
hiyo na kuwatoa nje wamiliki wa nyumba hiyo na kuondoka na vyombo vyao
vya ndani wakidai nyumba hiyo imeshauzwa kwa , Thobias Ludovick Senya
baada ya mmiliki kushindwa kulipa deni la shilingi million 3.7 alilokuwa
akidaiwa na taasiai ya fedha Heritage.
Baada ya tukio hilo familia hiyo yenye watu wapatao kumi wakiwemo watoto
na kichanga walianza kulala nje kando ya geti la nyumba hiyo wakipigwa
na baridi kali pasipo kuwa na msaada wowote
Mmiliki wa nyumba hiyo Josephat Nehemia Ogaga alisema baada ya familia
yake kutolewa nje wakati yeye akiwa safarini walikuja walinzi hao wa
kampuni ya kifaru na kuanza kulinda na baada ya yeye kurejea alifanikiwa
kuwaondoa walinzi hao na kuirejesha ndani familia yake akidai taratibu
za kuuza nyumba yake hazikufuatwa ila kilichofanyika ni uhuni .
“Nikweli nilikuwa nadaiwa na Heritage financial shilingi milioni 3 .7 na
nililipa deni na kubaki shilingi million 1.8 hivyo hatua ya kuja kuuza
nyumba yangu yenye thamani shilingi million 200 kwa deni hilo ni uhuni
mtupu umefanyika” alisema Nehemia
Hata hivyo siku moja baadae walinzi hao walirejea tena wakiwa na silaha
za moto na kuanza kufyatua risasi ovyo ndani ya nyumba hiyo kwa lengo la
kuwatisha familia hiyo ili waondoke ndani ya nyumba hiyo ambapo moja ya
risasi ilimjeruhi mwanafunzi huyo kichwani ambaye amelazwa katika
hospitali ya rufaa ya KCMC Mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya matibabu
Kamanda Mkumbo amezitaka kampuni za ulinzi kutoingilia migogoro bila
kufuata utaratibu kwani vyombo vyenye mamlaka ya kushughulikia migogoro
kama hiyo vipo na hivyo amezitaka kampuni za ulinzi kufuata taratibu zao
za utendaji wa kazi na kuacha kukimbilia maslahi yao ya kupata fedha
haraka,
Mkumbo alisema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu shitaka linalomkabili.
0 comments:
Post a Comment