Mahakama
ya Wilaya ya Ilala, imemhukumu Shabani Huseni (29), kifungo cha miaka
30 jela, baada ya kupatikana na hatia ya kunajisi mtoto wa miaka tisa.
Akisoma
hukumu hiyo jana Hakimu Mkazi Catherine Kihoja alisema upande wa
mashitaka ulipeleka mashahidi watano ambao wameweza kuthibitisha
mashitaka bila kuacha shaka yoyote.
“Kutokana
na ushahidi uliotolewa mahakamani hapa umeweza kuthibitisha mashitaka
hivyo, mshitakiwa ninamtia hatiani kama alivyoshitakiwa,’’alisema Hakimu Kioja.
Kabla
ya kutolewa kwa adhabu hiyo Wakili wa Serikali, Neema Moshi, aliomba
mahakama kutoa adhabu kali kwa mujibu wa sheria kwa kuwa mtoto
aliyefanyiwa kitendo hicho ameathirika kisaikolojia na kupata madhara
kiafya kutokana na kutokwa na harufu mbaya sehemu zake za siri.
Aidha, mshitakiwa aliomba mahakama impunguzie adhabu kwa kile alichodai kwamba hana ndugu, ombi ambalo lilitupiliwa mbali.
Inadaiwa
kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo tarehe isiyofahamika Julai mwaka
jana eneo la Kipunguni B, Moshi Baa wilayani Ilala ambapo alimbaka mtoto
wa miaka tisa.
0 comments:
Post a Comment