JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linawashikilia watuhumiwa 200 wanaohusishwa na makosa mbalimbali.
Wanne
kati ya hao, wanatuhumiwa kukutwa na gari lililoibwa hivi karibuni
katika eneo la ofisi za Mamlaka ya Udhibiti wa Bima Tanzania (TIRA)
zilizopo Manispaa ya Ilala.
Mkuu
wa Operesheni Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya, alitaja
watu hao wanne wanaotuhumiwa kukutwa na gari hilo kuwa ni Leonard Said,
Omary Said, Shomaly Kilobo na Adam Unemba.
Alisema
katika uchunguzi wa awali, watuhumiwa wote wamekiri kuhusika katika
wizi wa gari hilo, aina ya Toyota Spacio lenye namba za usajili T 398
CAE, boksi la chuma la kutunzia fedha na televisheni ya ukubwa wa inchi
32.
Alisema
Desemba 5, mwaka huu alipokea taarifa kutoka kwa Mhasibu Mkuu wa TIRA,
Egnance Edward (53) kuwa wamekuta ofisi za mamlaka hiyo, zimevunjwa na
kuibwa baadhi ya vifaa ikiwemo gari hilo.
0 comments:
Post a Comment