TAARIFA KWA UMMA
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) linapenda kutoa ufafanuzi kwa
umma, juu ya vijana waliohitimu kidato cha sita mwezi Mei mwaka 2016 na
kutakiwa kujiunga na mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria Opereshani
Magufuli awamu ya pili.
Vijana wa Mujibu wa Sheria wanaotakiwa
kuripoti kwenye makambi ya JKT waliyopangiwa ni wale wanafunzi wote
waliomaliza kidato cha sita mwezi Mei mwaka 2016, ambao hawakuchaguliwa
kwenye mafunzo ya JKT Mujibu wa Sheria Operesheni Magufuli awamu ya
kwanza na hawakupata nafasi ya kujiunga na vyuo vya elimu ya juu.
Iwapo kuna muhitimu yeyote ambaye jina
lake limetajwa kwenye orodha ya vijana wanaotakiwa kujiunga na mafunzo
ya JKT Mujibu wa Sheria Operesheni Magufuli awamu ya pili na tayari
ameshajiunga na chuo cha elimu ya juu, anatakiwa kuandika barua ya
kuomba kuhairisha kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria,
akiambatisha vithibitisho vya yeye kuwa mwanachuo wa chuo cha elimu ya
juu.
Barua hiyo itumwe kwa Mkuu Jeshi la
Kujenga Taifa, Makao Makuu ya JKT, Sanduku la Posta 1694, Dar Es Salaam
au iwasilishwe kwa mkono Makao Makuu ya JKT.
Aidha, JKT inaukumbusha umma tena, hatua
kali za kisheria zitachukuliwa kwa kijana yeyote ambaye amechaguliwa
kujiunga na mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria Operesheni Magufuli
awamu ya pili na amekaidi kuhudhuria mafunzo hayo bila ya sababu
zilizotajwa hapo juu.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya JKT
Tarehe 13 Desemba 2016
0 comments:
Post a Comment