Rais
wa Jamhuri ya Muungano Tanzania,Dk.John Pombe Magufuli,amefichua siri
ya kusali Krismasi kwenye kanisa la Parokia ya Moyo wa Yesu, mjini
Singida mwaka huu.
Ametaja
siri hiyo kuwa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita, aliwahi
kusali kwenye kanisa hilo na wakati akitoka, alikutana na sista mmoja
(hamkumbuki jina) ambaye alimzawadia rozali, na kumwahidi kuwa itamsadia
kushinda uchaguzi huo.
Rais
Magufuli ametoa siri hiyo jana wakati akizungumza kwenye sherehe ya
Krismasi iliyofanyika kwenye kanisa la Porokia ya Moyo wa Yesu, na
kuhudhuriwa pia na mke wa Rais, Mama Janeth Magufuli.
Akifafanua,
alisema kuwa rozali hiyo amezunguka nayo kwenye kampeni yake, na mwisho
wa siku, alifanikiwa kupata kura za kutosha na hivyo kuwa mshindi.
“Hiyo
ndio sababu kubwa au siri ya mimi kufika mjini Singida, na kuungana na
wakazi wa mkoa wa Singida na Watanzania kwa ujumla, kusherehekea
kuzaliwa kwa Yesu kristo,” alisema na kusababisha mamia ya waumini kushangilia kwa nguvu.
Rais
Magufuli alitumia fursa hiyo kuwataka Watanzania wote kutumia sikukuu
hii ya Krismasi kuimarisha upendo, kuvumiliana na wala wasibaguane ,na
kwa njia hiyo,Tanzania itaendelea kupaa kimaendeleo.
Katika
hatua nyingine, alisema kuwa Watanzania na hususani wakulima,
wahakikishe wanazitumia vizuri mvua zinazonyesha kwa sasa nchini kwa
kuchapa kazi ya kilimo kwa nguvu zote na kulima mazao yanayostahimili
ukame.
“Ndugu
zangu waumini na Watanzania kwa ujumla, acheni kulialia kuwa fedha
zimepotea … fedha hazijapotea isipokuwa ninyi wenyewe hamfanyi kazi.
Vitabu vyote vya madhehebu ya dini vinasisitiza wajibu wa kuchapa kazi …
na vinasema asiyefanya kazi na asile,” alisisitiza.
Akiijengea
nguvu hoja yake ya hapa ni kazi tu, alisema kuwa Yesu kristo amezaliwa
na fundi mchapa kazi kweli kweli seremala, na hivyo tunaposherehekea
Krismasi Watanzania wote wenye uwezo wa kufanya kazi, wafanye kazi huku
wakijua hakuna cha bure.
Aidha,
Rais Magufuli, aliwataka wakazi wa mkoa wa Singida, kuongeza uzalishaji
wa zao la alizeti, ili kukiwezesha kiwanda kikubwa cha kukamua mafuta
ya alizeti cha Mount Meru kupata mbegu za kikudhi mahitaji ya kiwanda.
Awali
askofu wa kanisa katoliki jimbo la Singida, Edward Mapunda, alitumia
fursa hiyo kuwakumbusha wakazi wa mkoa wa Singida, kutunza mazingira,
ili yaweze kuwatunza na wao.
Alisema
hivi sasa hali ni mbaya kutokana na binadamu kuongeza kasi ya kuharibu
mazingira, kitendo kinachochangia madhara mengi ikiwemo uhaba wa mvua.
“Mimi
nashangaa sana, watu wanaendelea kuzaa huku wakiendelea kuharibu
mazingira na kutishia nchi kuwa jangwa. Tuna zaa watoto waje wateseke
kutokana na uharibifu wa mazingira. Kama tunaendelea kuharibu mazingira,
ni vema tuache kuzaa”, alisema Mapunda.
0 comments:
Post a Comment