December 15 2016 Waziri wa elimu, sayansi na teknolojia Prof. Joyce Ndalichako alikutana
Dodoma na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu ili kujadili namna sahihi
ya kuboresha sekta hiyo katika kipindi cha awamu ya tano ambapo katika
baadhi ya vitu alivyogusia ni pamoja na suala la ajira kwa walimu.
Waziri Ndalichako amesema…>>>’Utaratibu
wa kuajiri tunauboresha, zamani ilikuwa ukisoma ualimu unapangiwa
sehemu ya kazi bila hata kuhakikiwa lakini sasa ni lazima kila
anayemaliza mafunzo ahakikiwe kwanza ndipo hatua zingine zinafuatwa‘ –Pro. Joyce Ndalichako
‘Tumebaini
kwamba serikali imekuwa ikipoteza fedha nyingi kwa kuajiri watu
wasiokuwa na sifa, tayari katibu mkuu wa wizara yangu ameshatoa tangazo
kwa wahitimu wote waliomaliza mafunzo ya sayansi mwaka 2015 wawasilishe
vyeti vyao ili vihakikiwe‘ –Pro. Joyce Ndalichako
‘Na
wale watakaoonekana wana vyeti visivyokuwa na mashaka ndio watakaopata
nafasi kwahiyo zoezi la ajira kwa walimu limeanza hivyo tunaamini tatizo
la ajira kwa walimu haliakwisha lakini tutakuwa tumelipunguza kwa
nafasi kubwa‘ –Pro. Joyce Ndalichako
unaweza kuendelea kumsikiliza Pro. Joyce Ndalichako kwenye hii video hapa chini…
BAADA
ya kusitisha ajira za umma kwa takribani miezi tisa, hatimaye serikali
imetangaza ajira kwa wahitimu wa ualimu kwa shule za sekondari.
Hata hivyo, ajira mpya zilizotangazwa na serikali jana, zinawahusu
walimu wa ngazi ya stashahada na shahada ya ualimu wa masomo ya sayansi
na hisabati kwa shule za sekondari.
Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya
Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Maimuna Tarish, na
kuchapishwa kwenye tovuti rasmi ya wizara hiyo, serikali inatarajia
kuajiri walimu wa masomo ya sayansi na hisabati kwa shule za sekondari
waliohitimu mwaka jana.
Hata hivyo, idadi ya walimu wanaohitajika kwa ajili ya kufundisha masomo
hayo haikuelezwa katika tangazo hilo. "Ajira hii ni kwa walimu wa
stashahada na shahada za mafunzo ya ualimu wa masomo ya hisabati na
sayansi waliohitimu mwaka 2015.
Wahitimu hao wanatakiwa kuwasilisha nakala za vyeti vyao vya elimu ya
sekondari (kidato cha nne na sita) na taaluma ya ualimu (stashahada na
shahada) kwa ajili ya uhakiki.
"Nakala hizo ziwasilishwe kupitia barua pepe ya wizara info@moe.go.tz kuanzia tarehe ya tangazo hili (jana) hadi Ijumaa Desemba 16, 2016.
Yeyote ambaye vyeti vyake havitahakikiwa, hatafikiriwa katika ajira,"
tangazo hilo lilieleza. Katika mwaka huu wa fedha, serikali imepanga
kuajiri watumishi 71,496 kwenye sekta mbalimbali zikiwamo elimu, afya na
viwanda.
0 comments:
Post a Comment