Serikali imesema inaanza uhakiki upya, kwa kupitia fomu zote za maombi
zilizowasilishwa na wanafunzi kwenye bodi ya mikopo, baada ya kubaini
kuwa idadi kubwa ya wanafunzi walioomba mikopo ya elimu kupitia bodi ya
mikopo nchini wamejaza taarifa za uongo.
Profesa Simon Msanjila ambaye ni Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia amesema haya wakati wa mahafali ya nne ya Chuo
Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mbeya , akisema serikali imeanza
uhakiki mara moja kwa kupitia fomu zote zilizowasilisha kwenye bodi ya
mikopo , na atakaye bainika kuwa amejaza taarifa zisizo sahihi
atafikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Katika mahafali haya wanafunzi zaidi ya 800 wanehitimu kozi mbalimbali
zikiwemo za uhandisi, usanifu wa majengo, umeme na tehama.
Awali Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya Profesa Mark
Mwandyosa ameandaa mhadhara ulioshirikisha wanazuoni na wasomi
mbalimbali ,na kumtaka Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Joseph
Msambichaka kufundisha watanzania sayansi na teknolojia, na sio
teknolojia pekee, ili kuandaa wanasayansi ukilinganisha na wahitimu
wengi wanaohitimu chuoni hapo ambao wanajikita zaidi kwenye teknolojia.
0 comments:
Post a Comment