Mwanazilishi
wa Mtandao wa JamiiForums aliyekamatwa na Polisi kuanzia juzi Maxence
Melo, leo amefikishwa mahakamani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisitu
Jijini Dar es Salaam leo asubuhi na kusomewa mashtaka matatu.
Melo
amefikishwa mahakamani leo ikiwa ni baada ya sitofahamu kubwa iliyokuwa
imetanda kuhusu kosa hasa la kukamatwa kwake ambapo tangu alipokuwa
amekamatwa zaidi ya saa 24 zilizopita hakuwa amefikishwa mahakamani huku
Polisi wakiwa wamefanya upekuzi ofisini kwake na nyumbani.
Maxence
Melo amepandishwa kizimbani leo na kusomewa mashtaka matatu
yanayomkabili likiwemo la kumiliki na kuendesha tovuti ambayo
haijasajiliwa hapa nchini Tanzania (JamiiForums).
Mashtaka
mengine ni kuzuia na kuharibu taarifa ambazo Jeshi la Polisi wamekuwa
wakizitaka kwa ajili ya uchagunguzi chini ya kifungu cha 22 cha Sheria
ya Makosa ya Mitandao na kushindwa kutoa ushirikiano kwa Jeshi la
Polisi na kuharibu uchunguzi chini ya kifungu cha namba 22 cha Sheria
ya Makosa ya Mitandao.
Kwa
mujibu wa taarifa zilizokuwa zimetolewa na tovuti ya JamiiForums jana,
walisema kuwa ‘server’ ya tovuti yao haipo nchini Tanzania wala barani
Afrika lakini hawakutaja ni nchi gani ilipo.
Melo
apelekwa rumande Keko hadi Jumatatu Disemba 19 mwaka huu baada ya
kukosa mdhamini katika shtaka la tatu la kumiliki na kuendesha tovuti
ambayo haijasajiliwa nchini.
0 comments:
Post a Comment