Serikali
imesema kumeibuka upya kwa ugonjwa wa kipindu pindu katika mikoa sita
ambapo takwimu zinaonyesha kuwa wapo wagonjwa 458 huku sita wakiwa
wameshapoteza maisha kutokana na ugonjwa huo.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na watoto Mh. Ummy Mwalimu aliitaja mikoa yenye wagonjwa wa
kipindipindu kuwa ni pamoja na Morogoro wagonjwa 282 na Dodoma wagonjwa
96.
Aliitaja
mikoa mingine kuwa ni Mara wagonjwa 31, Kigoma wagonjwa 30, Arusha 11
na katika jiji la Dar es salaam wapo wagonjwa 8 wa kipindupindu kati ya
hao 6 kutoka Ubungo na 2 kutoka Ilala.
Aidha,
Mh. Waziri amebaini kuwepo kwa uzembe mkubwa unaofanyika katika wilaya
na mikoa kwa kushindwa kutoa taarifa za ugonjwa huo huku wagonjwa wa
kipindu pindu wakilazwa pamoja na wagonjwa wa kawaida kwa kile
kinachoelezwa ni viongozi kuogopa kutumbuliwa na Rais Dkt. John
Magufuli.
0 comments:
Post a Comment