Mshambuliaji
wa timu ya vijana ya Mbao FC U-20 Ismail Mrisho Khalfan anayevalia jezi
nambari 4 amefariki Dunia jana jioni baada ya kuanguka uwanjani
Kaitaba wakati wa mtanange wao dhidi ya timu ya vijana wa Mwadui FC
ikiwa ni mechi ya mwisho ya kumaliza duru la kwanza la ligi ya Vijana.
Ismail Khalfan alifariki baada ya kufikishwa Hospitali ya Serikali ya mjini Bukoba.
Ismail
Khalfan kabla ya kufikiwa na umauti aliweza kuifungia timu yake bao la
kwanza na bao la pili lilifungwa kwa mkwaju wa Penati hivyo mtanange
kumalizika kwa 2-0.
Kabla
ya kuanguka Ismail aligongana na beki wa Mwadui FC na baadae akiwa
peke yake alianguka chini lakini akainuka halafu akaanguka tena na
kutokana na ukosefu wa huduma ya kwanza na gari la wagonjwa katika
Uwanja wa Kaitaba kulipelekea marehemu kupandishwa kwenye gari la zima
moto na kupelekwa hospital ambapo mauti yalimkuta.
0 comments:
Post a Comment