WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi,
Charles Tizeba kufanya uchunguzi kwa nini mbolea ya minjingu
inayozalishwa nchini haitumiki na badala yake inaagizwa mbolea kutoka
nje ya nchi.
Ametoa
agizo hilo Jumamosi, Desemba 3, 2016 wakati alipotembelea kiwanda cha
Fibre Board 2000 Limited ambacho kinatengeneza bidhaa mbalimbali ikiwemo
mbolea ya Minjingu, wakati akiwa katika siku ya pili ya ziara yake ya
kikazi mkoani Arusha.
Alisema
mbolea hiyo licha ya kuwa na viwango vya ubora vinavyohitajika,
haitumiki nchini kwa sababu ya kuingiliwa na masuala ya kisiasa dhidi ya
matumizi yake.
“Nchi
jirani ya Kenya inaiona mbolea hii bora kuliko sisi wa ndani?
Mheshimiwa Waziri wa Kilimo are we serious? Tunazalisha mbolea hapa
tunasema haina kiwango lakini Kenya wanaitaka na wameagiza tani
300,000,” alisema.
Waziri
Mkuu aliongeza kuwa “Jambo hili lazima liangaliwe ndani ya Wizara kwa
nini mnaagiza mbolea kutoka nje wakati ndani tunazalisha hii ni mianya
ya rushwa, rushwa ulaji ulaji tu. Waziri lichukulie maanani jambo hili
hatutaki siasa katika sekta ya kilimo,”.
Alisema
kumekuwa na mijadala mingi kuhusu mbolea ya minjingu kumbe baadhi ya
watendaji wanatengeneza mianya ya kwenda kununua mbolea nje ambako
hutumia fedha nyingi ambazo zingeweza kutumika katika miradi mingine ya
maendeleo.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa kiwanda cha Fibre Board 2000 Limited, Tosk
Hansi amesema kampuni hiyo inayozalisha bidhaa mbalimbali ikiwemo mbolea
ya minjingu, imetoa ajira kwa watu zaidi ya 1,800 wengi wao wakiwa ni
vijana ila inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ya urasimu wakati
wanapoomba vibali vya uvunaji mazao ya misitu.
Awali,
kampuni hiyo ya Fibre Board 2000 limited imemkabidhi Waziri Mkuu
mchango wa madawati 1,000 kwa ajili ya shule mbalimbali za mkoani Arusha
ili kuwawezesha wanafunzi kusoma katika mazingira mazuri.
0 comments:
Post a Comment