TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya e -
Government Agency (eGA) anatarajia kuendesha usaili na hatimaye
kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili.
Wasailiwa walioitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia yafuatayo:
1. Ukaguzi wa vyeti utafanyika saa 1:00 kabla ya muda wa mtihani wa
mchujo kuanza.
2. Kwa wale wasiokuwa na mtihani wa mchujo usaili utaanza saa moja
kamili asubuhi (1:00) na utafanyika mahali na tarehe kama inavyoonesha
katika nafasi husika.
3. Kuja na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi mfano: kitambulisho cha
mkazi, kupigia kura, kazi, hati ya kusafiria n.k
4. Kuja na Vyeti Halisi (original certificates) vya kuanzia kidato cha nne,
sita, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana
na sifa za mwombaji.
5. “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati
matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS
SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
6. Kila msailiwa aje na picha moja (Passport size).
7. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.
18. Kila msailiwa azingatie tarehe na eneo alilopangiwa kufanyiwa usaili
9. Kila msailiwa aje na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate)
10. Kwa wale waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao
vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU & NECTA)
11. Wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue
kuwa maombi yao hayakufanikiwa na wasisite kuomba tena mara nafasi za
kazi zitakapotangazwa.
12. Kada zenye mchujo, wasailiwa watakaofaulu mtihani wa mchujo
wazingatie mahali na tarehe za usaili wa mahojiano kama ilivyooneshwa
kwenye tangazo. BONYEZA HAPA KUANGALIA MAJINA HAYO
MAJINA MENGINE BONYEZA HAPA
0 comments:
Post a Comment