Rais Jakaya Kikwete amesema serikali imetenga kwa kila halmashauri ya
wilaya nchini kupatiwa shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa
nyumba za walimu ili kuwapunguzia adha na usumbufu walimu wanapopangiwa
kwenda katika vituo vya kazi wanakosa mahali pa kuishi.
Rais Kikwete ametoa ahadi hiyo wakati akizungumza na viongozi wa
serikali,chama na wananchi wa tarafa ya Kimbe iliyopo wilayani Kilindi
wakatia akifungua maabara zinazojengwa chini ya sera ya kutaka kila
shule ya sekondari iwe na maabara ili kuwanufaisha wanafunzi waweze
kusoma masomo ya sayansi kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla.
Kuhusu ujenzi wa shule za kata ambao amedai kuwa awali zoezi hilo
lilipuuzwa na kuitwa shule za yebo yebo,rais Kikwete amesema ni shule
zinazowaunganisha Watanzania tofauti na awali wanafunzi kufaulu ilikuwa
ni kwa baadhi ya shule nandio maana serikali imeanza kujenga shule hizo
kisha kusomesha idadi kubwa ya walimu ikifatiwa na maabara ili kuweka
uwiano kielimu nchini.
Awali akielezea changamoto wanazokabiliana nazo wakazi wa tarafa ya
Kimbe wilayani Kilindi,mbunge wa jimbo hilo mheshimiwa Beatrice
Shelukindo amesema wakazi wa eneno hilo wanalazimika kuuza debe moja la
mahindi kwa shilingi 2,400/= hivyo amemuomba rais Kikwete kuwashawishi
hifadhi ya taifa ya chakula kununua mazao yao ili kunusuru nguvu za
wakulima zisipotee bure
0 comments:
Post a Comment