BASI LA AM COACH LAPINDUKA WILAYANI MASWA NA KUJERUHI WATU WATATU
Basi la AM Coach likiwa eneo la tukio katika kijiji cha Sayusayu wilayani Maswa mkoani Simiyu |
Watu watatu wamejeruhiwa vibaya katika ajali ya Basi la AM Coach lililokuwa linatokea katika kijiji cha Sayusayu wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu kuelekea jijini Mwanza
Abiria
hao ni miongoni mwa abiria 54 waliokuwa katika Basi hilo lenye namba za
Usajiri T607 AQN lililokuwa likitoka wilayani Meatu mkoani Simiyu
kuelekea Jijini Mwanza.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Simiyu Charles Mkumbo amesema kuwa ajali hiyo
imetokea leo majira ya saa 3:00 asubuhi wakati Basi hilo likitokea mjini
Mwanhunzi wilayani Meatu kuelekea Jijini Mwanza mara baada ya kuacha
njia na kuparamia mti na kupinduka.
Amesema
dereva wa gari hilo Ismail Hassan (46) mkazi wa Mwanza alishindwa
kulimudu basi hilo wakati akipishana na roli moja ya mizigo linalodaiwa
kukatalia katikati ya barabara na kusababisha dereva wa basi kushindwa
kumudu gari lake.
Akielezea
hali ya abiria waliojeruhiwa Mkumbo amesema kuwa watu watatu hali zao
ni mbaya wamekimbizwa katika hosptali ya rufaa ya Bugando jijini Mwanza.
Kamanda
huyo amewataja abiria waliojeruhiwa vibaya kuwa ni Pili Abrahim
(54)mkazi wa eneo la Mbugani jijini Mwanza ambaye amevunjika mkono wake
wa kushoto na kichwani na mtoto wake wa kike Kwangu Daniel (5) aliyekuwa
akisafiri na mama yake kwenda Bugando kwa uchunguzi zaidi wa daktari
wake baada ya kuvunjika mguu wa kulia na katika ajali hiyo amevunjika
mkono wa kushoto.
Pia
mama wa mtoto huyo Mwalu Jilala (32)wote wakazi wa kijiji cha Somanda
wilayani Maswa amevunjika mkono wa kushoto,michumbuko na maumivu makali
sehemu ya kifua na kiuno.
Wengine
katika ajali hiyo ambao wamelazwa katika hopitali ya wilaya ya Maswa ni
Aziza Shaaban(42) mfanyabiashara na mkazi wa Ibaga wilaya ya Mkalama
mkoani Singida ambaye amejeruhiwa sehemu za kichwani na kukatwa na kitu
chenye ncha kali katika mikono wa kushoto,Madaraka Daudi (34)mkazi wa
kijiji cha Bushingwamala wilayani Busega na Abel Yohana (27)mkazi wa
Maswa na walimu wa nyimbo za injili aliyekuwa anakwenda kurekodi nyimbo
jijini Mwanza.
Naye
mmoja wa abiria aliyenusurika katika ajali hiyo Happines Mgugu(41)mkazi
wa Mbugani jijini Mwanza Ambaye pia ni wifi waPili Abrahim amesema basi
hilo lilikuwa katika mwendo kasi na ghafla katika moja ya kona
lilikutana na roli moja la mizigo likielekea mjini Maswa ambalo
halikupisha njia na kung’ang’ania katikatika ya barabara na kusababisha dereva wa basi kulikwepa na kwenda kuparamia mti na gari hilo kupinduka.
CREDIT:Samwel Mwanga-Simiyu
0 comments:
Post a Comment