KUNA STAA wa sinema za Bongo na Miss Tanzania 2006, Wema Isaac Sepetu ‘ameingizwa mjini’ na mhariri wa filamu Bongo mwenye asili ya Kiarabu aliyejulikana kwa jina moja la Chidy kwa kuingia mitini na shilingi 5,000,000 alizompa ili azihariri filamu zake mbili lakini kazi haikufanyika.
Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi Tanzania Kituo Kikuu jijini Dar es Salaam, kilisema ilikuwa mwaka jana (2013) ambapo Wema alimkabidhi mhariri huyo filamu mbili, Super Star na Vian Unaspect.
MALIPO YAFANYWA, KAZI HAKUNA
Ikazidi kudaiwa kwamba mbali na filamu hizo, Wema alimlipa jamaa shilingi 2,500,000 ili kuzihariri (editing) filamu hizo ikiwa ni hatua ya mwisho kabla ya kuingia sokoni.
JAMAA AINGIA MITINI, AMKWEPA WEMA
Habari zikazidi kudai kwamba, baada ya kuudaka ‘mpunga’ huo jamaa huyo amekuwa akimzungusha Wema kufanya kazi zake na kumkabidhi ili azipeleke sokoni ndipo wiki iliyopita mlimbwende huyo akalazimika kwenda kutoa taarifa kwenye Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’ jijini Dar es Salaam.
GHARAMA ZA FILAMU
Kwa mujibu wa mtoa habari huyo, alimsikia Wema akisema filamu zote zimemteketezea shilingi milioni 70,000,000 mbali na hizo alizomlipa huyo mhariri wa filamu ambazo zikiingizwa kwenye gharama nzima inafika shilingi 75,000,000.
KAMA ZINGEINGIA SOKONI
Habari zaidi zinasema kwamba kama filamu hizo zingehaririwa mwaka jana na kuingizwa sokoni, Wema angekunja mkobani kiasi cha shilingi 140,000,000 hivyo kurudisha gharama za kuandaa (75,000,000) na faida juu (65,000,000).
WEMA ASWAKWA, AKATAE AU AKUBALI
Kufuatia maelelezo hayo kutoka chanzo chetu, mwishoni mwa wiki iliyopita, Uwazi lilimsaka mrembo huyo ili afunguke kuhusu kuwepo kwa madai hayo, alipopatikana na kuulizwa sakata zima hakuwa tayari kupepesa macho, akakiri.
Alisema awali kijana huyo aliyemdhulumu alikuwa mfanyakazi wake katika kampuni ‘mufilisi’ ya Endless Fame, cha ajabu toka ampatie hiyo kazi ya kumtengenezea pamoja na kumkabidhi fedha amekuwa akimchenga toka mwaka jana.
“Mimi nashindwa hata kumuelewa ana dhumuni gani na hizo kazi zangu maana hapo ana kama shilingi milioni 140 zangu, kwa kuwa kila kazi nilikuwa nalipwa shilingi milioni 70, nilishafanya makubaliano na Kampuni za Proin Promotion na Steps kuwapa filamu zangu lakini yeye ananizungusha, toka kipindi kile sijaende China, nikimuuliza majibu yake siyaelewi.”
WEMA AMWAGA CHOZI, MTUHUMIWA MBARONI
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Wema aliendelea kulalamika mpaka kufikia hatua ya kumwaga chozi:
“Juzi kati Mtitu alitaka nifanye naye kazi lakini akanikumbushia Filamu ya Super Star, kwamba hajaiona sokoni mpaka sasa, ndipo nikamuelezea, akasema hawezi kukubali niipoteze kirahisi, lazima nisimame kidete kuipata ndiyo nikaenda naye mpaka Kituo cha Polisi Mabatini kufungua kesi na Chidy akakamatwa siku hiyo hiyo.”
APEWA SIKU SABA
Wema aliendelea kusema: “Polisi walimpa siku saba ahahakikishe ananikabidhi kazi zangu pamoja na kompyuta moja ambayo aliichukua ofisini kwangu bila ridhaa ya mimi mwenyewe na akagoma kuirudisha.”
AFISA WA POLISI
Naye afisa mmoja wa polisi wa kituo hicho ambaye alizungumza na gazeti hili kwa sharti la kutoandika jina lake gazetini alithibitisha Wema kufungua kesi Mabatini na ikapewa jalada Namba KJN/RB/5850/14 WIZI WA KUAMINIWA 3/7/2014.
“Ukweli ni kwamba zikipita siku saba bila kijana huyo kuleta fedha na kompyuta ya Wema hapa polisi, tutamsaka na tukimkamata sheria itachukua mkondo wake,” alisema afisa huyo wa polisi.
UPER STAR, OMOTOLA ALIFIKA
Kama itakumbukwa sawasawa Filamu ya Super Star ilizinduliwa Juni 24, 2012 kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar na nyota wa muvi za Nollywood (Nigeria), Omotola Jalade Ekeinde alishiriki.
0 comments:
Post a Comment