Baa ya ndani ya Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhad Mussa Salum (pichani kushoto), amewavaa baadhi ya mastaa Waislamu wa Kibongo wenye kaunta zenye pombe majumbani mwao hasa kwa kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani huku akiwataka waondoe mara moja kwani ujana unawasumbua,

Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhad Mussa Salum
WAMO DIDA, WEMA & DIAMOND
Uchunguzi wa paparazi umebaini kwamba baadhi ya mastaa Waislamu wenye kaunta zenye pombe majumbani mwao kuwa ni pamoja na Mtangazaji wa Radio Times FM, Hadija Shaibu ‘Dida’, staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ na msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul

‘Diamond Platnumz’.
Akizungumza na paparazi wiki hii jijini
Dar es Salaam, Shehe Salum alisema kwamba, kwanza ameshtushwa na habari
ya hao wanaojiita mastaa kuwa na kaunta za pombe majumbani kwao kwani
ni habari ngeni masikioni mwake na kusema kuwa kwa semina wanayoipata
mwezi huu hawatakiwi kutenda maovu.
WANAPASWA KUOMBA DUA
Alisema kuwa mastaa hao wanapaswa kuutumia Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kusoma Quran, kuomba dua na kuacha maovu yote.

“Hao mastaa wenye kaunta wanatakiwa
kuacha na kuondoa kabisa kwani Ramadhani imeletwa kwetu kama semina na
hatutakiwi ikiisha turejee kule tulipokuwa.
“Mafunzo ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani
maana yake tujifunze na tuachane na kule tulikotoka, hivi kwa nini
wasijiulize mastaa wenzao wako wapi kwa mfano Sharo (mchekeshaji
Sharomilionea) na wengine waliotangulia mbele ya haki?
WANAKULA UJANA?
“Wasijidanganye na ujana walio nao, wakikutwa na mauti, mbele ya haki watasema nini?
“Nawaasa kutorudi nyuma na kujifunza kwelikweli namna ya kuishika dini na nguzo zake,” alisema shehe huyo.

SWAUMU ZAO VIPI?
Shehe mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake anayeswalisha katika msikiti uliopo Sinza jijini Dar alisema:
“Kiukweli kabisa pombe ni haramu na hatutakiwi kuikaribia hata kidogo. Hawa ambao wamefikia hatua ya kuwa na kaunta za pombe majumbani kwao, wanakosea sana.

“Kwa mfano mwezi huu mtukufu kama
wanafunga, si kwamba hawapati thawabu, wanapata ila kwenye kuikaribia
pombe, watakuwa wanapata dhambi.
“Kwa hiyo unaweza kuwa umefunga lakini
ukashangaa mpaka mwezi umeisha thawabu zako zimepungua kutokana na mambo
mengine yanayokufanya upate dhambi.”
DIDA ANASEMAJE?
Baada ya Shehe Salum kuwavaa mastaa hao, paparazi lilimsaka mmoja baada ya mwingine.
Alipopatikana, Dida ambaye ni binti wa Kiislamu mwenye kaunta ya pombe nyumbani kwake, Mwananyama, Dar alikuwa na haya ya kusema:

“Ni kweli mimi nina kaunta ndani kwangu
lakini kwa mwezi huu hata mimi naichukia sana pombe na sipendi kabisa
kuiona pamoja na kwamba sijui sana sheria za dini japo ni muhimu kuzijua
nguzo zake.
“Hata mimi kama binti wa Kiislamu kwa mwezi huu mtukufu sinywi pombe na hiyo kaunta ni kwa ajili ya wageni wangu wanaonitembelea.”

NYUMBANI KWA DIAMOND
Wiki mbili zilizopita ishu hiyo ilitibua futari nyumbani kwa Diamond maeneo ya Sinza-Mori, Dar hivyo kulazimika kuondoa pombe kali zilizokuwa zimejazwa kwenye kaunta.

WEMA VIPI?
Kwa upande wake Wema ambaye ukiingia kwake kitu cha kwanza unakutana na kaunta ya pombe na vinywaji vingine alipotafutwa ili kuzungumzia ishu hiyo, simu yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa.

0 comments:
Post a Comment