Nao
wazazi ambao waliambatana na watoto wao hadi ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Mbeya, Abbas Kandoro na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’
(CHADEMA) kwa nia ya kutafuta suluhu ya suala hilo, walisema kuwa tangu
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kutangaza majina ya wanafunzi
waliofaulu kwa ajili ya kidato cha tano na shule walizopangiwa, hakuna
majina ya watoto wao.
Mmoja
wa wazazi hao, Lawrance Shimo, alisema baada ya kufuatilia kwa kina
ikiwemo kuuliza uongozi wa shule, walibaini kuwa katika shule hiyo
hakuna mwanafunzi hata mmoja aliyepangiwa shule kwa ajili ya kuendelea
na kidato cha tano, licha ya kuwa na ufaulu wa alama mzuri.
0 comments:
Post a Comment