Wednesday, 9 July 2014

MCHEZAJI WA UJERUMANI MIROSLAV KLOSE AWEKA HISTORIA KOMBE LA DUNIA

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Miroslav Josef Klose akishangilia baada ya kutupia bao la pili kwa Ujerumani usiku huu na kuvunja rekodi ya kupachika mabao.
Klose wakati akifunga bao lake la 16 katika michuano ya kombe la dunia.
Mkali wa mabao Miroslav Josef Klose.
MSHAMBULIAJI wa Ujerumani na timu ya Lazio ya Italia, Miroslav Josef Klose, ameweka historia usiku huu baada ya kutupia bao lake la 16 na kuwa mfungaji wa mabao mengi katika michuano ya Kombe la Dunia iliyoanza mwaka 1930 ambayo kwa sasa inaendelea nchini Brazil.
Klose ameifungia Ujerumani bao la pili wakati ikitoa kichapo cha mabao 7-1 dhidi ya Brazil katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Dunia 2014.
Klose alifunga mabao matano katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2002 na 2006, akatupia manne huko Afrika Kusini mwaka  2010 na mpaka sasa huko Brazil tayari amefunga mabao mawili moja dhidi ya timu yake na Ghana wakati la pili dhidi ya Brazil leo.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 36 amempiku mshambuliaji wa Brazil, Ronaldo Luís Nazário de Lima aliyekuwa na mabao 15.
Wachezaji wengine waliowahi kufunga mabao zaidi ya 11 kwenye michuano hiyo ni: Gerd Muller wa Ujerumani 14, Just Fontaine wa Ufaransa 13, Pele wa Brazil 12, Jurgen Klinsmann wa Ujerumani 11 na Sandor Kocsis wa Hungary 11.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger