picha ya pamoja |
WAZIRI wa Tamisemi, Hawa Ghasia, Julai 14, mwaka huu, amefungua
mkutano wa Viongozi wa Vyama vya Siasa vilivyokuwa na usajili wa kudumu
ngazi ya Taifa kujadili maoni ya wadau mbalimbali ya kuboresha kanuni
za uchanguzi wa viongozi wa mamlaka za serikali za mitaa unaotarajia
kufanyika Oktoba 2014.
Mkutano huo pia unahudhuriwa na Naibu Waziri wa Tamisemi, Aggrey
Mwanri, Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis na viongozi
wengine wa Wizara hiyo.
Kwa mujibu wa Waziri wa Tamisemi, mkutano huo unawapa fursa
viongozi wa vyama vya siasa ngazi ya Taifa kupitia hoja na maoni ya
wadau kama ilivyokwisha fanyika kwa makundi mengine.
Makundi ambayo yameshatoa maoni na ushauri wao ni Asasi za Kiraia
pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya nchini , maoni hayo na
ushauri utakaotolewa na Viongozi hao ambayo Serikali itayafanyia kazi
ili kupata kanuni bora za uchanguzi wa serikali za mitaa mwaka 2014.
Katika mkutano huo wa siku mbili viongozi mbalimbali wa vyama vya
siasa ngazi ya taifa wanashiriki akiwemo Mwenyekiti wa Taifa wa CUF,
Profesa Ibrahim Lipumba,pamoja na viongozi wengine wa vyama
mbalimbali vikiwemo vya Chadema, CCM, TLP na NCCR MAGEUZI.
0 comments:
Post a Comment