ZIKIWA zimekatika siku 40 tangu kifo cha muongozaji maarufu Bongo, George Otieno ‘Tyson’, mke wa ndoa wa marehemu, Yvonne Sheryl ‘Monalisa’, mama yake mzazi , Suzan Lewis ‘Natasha’ pamoja na mwanaye Sonia wamefanyiwa sherehe.
Katika shughuli hiyo ambayo ilihudhuriwa na mwandishi wa habari hizi, wafiwa hao waliingizwa bafuni na kuogeshwa kisha kuvalishwa nguo mpya na kutolewa nje, zoezi ambalo lilifanyika chini ya usimamizi wa mkongwe wa maigizo nchini, Zawadi.
Muongozaji wa shughuli hiyo, Mama Abdul
alisema nia ya kuwaosha wafiwa hao ni mila na desturi ya Kabila la
Kizaramo na kwamba wao kama marafiki wa karibu waliamua kuwafanyia
wenzao kwa lengo la kuwapa moyo baada ya kuwa kwenye matatizo.
Katika shughuli hiyo, Monalisa alishindwa kujizuia na kujikuta akiangua kilio, hali iliyosababisha hata mwanaye Sonia aungane naye, lakini mashosti zake walimtuliza.
Mama wa Monalisa, Natasha alisema: “Namshukuru sana Mungu kwa uwezo wake, kutujalia nguvu katika kipindi hiki kigumu kwa familia yetu, hasa mwanangu Monalisa na mwanaye Sonia.
0 comments:
Post a Comment