TBS KUPEWA KIBALI CHA KUAJIRI WAFANYAKAZI 200
Serikali inatarajia kutoa vibali vya kuajiri wafanyakazi
200 katika Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na zaidi ya asilimia 95 ya
wafanyakazi hao wataongeza nguvu katika kutayarisha na kusimamia
viwango vya ubora.
Hayo yalisemwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda, juzi wakati wa kufungua mkutano wa siku mbili wa Baraza la Wafanyakazi wa shirika hilo mjini Morogoro.Waziri Kigoda alisema Serikali inatambua umuhimu wa shirika hilo hapa
nchini hususan katika kuchangia uchumi wa nchi, kusimamia afya, usalama
na ustawi wa watu, kusaidia kuwalinda walaji, kuchangia biashara za
ndani na nje ya nchi na kusimamia ushirikiano wa Kimataifa katika nyanja
za viwango. Kwa mujibu wa Waziri huyo, changamoto kubwa zinazolikabili shirika hilo ambazo ni pamoja na uhaba wa watumishi, vifaa vya maabara, fedha
za maendeleo na matumizi ya kawaida, uelewa mdogo wa umma na Jumuiya ya
Wafanyabiashara juu ya dhana nzima ya viwango na ubora.
“Changamoto
hizi Serikali inazifanyia kazi na kwa mwaka ujao wa fedha kwa maana
2014/2015 ,Serikali inatarajia kuongeza wafanyakazi 200 ambao wengi wao watasaidia katika kuweka na kusimamia viwango,” alisema.Awali
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TBS, Profesa Cuthbert Mhilu,
alisema kwa mwaka wa fedha wa 2013/2014 , TBS ilipewa vibali vya kuajiri
wafanyakazi 45 na mwaka huu wa fedha wa 2014/2015 inatarajia kupewa
vibali vya kuajiri wafanyakazi wapatao 200 , zaidi ya asilimia 95 ya
wafanyakazi hao wataongeza nguvu katika kutayarisha na kusimamia viwango
vya ubora
0 comments:
Post a Comment