Na Frederick Katulanda, Mwananchi
Kwa mujibu wa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma,
Xavier Daudi nafasi hizo za kazi ambazo zinapatikana katika tovuti ya
Sekretarieti ya Ajira ya www.ajira.go.tz ni kwa ajili ya waajiri
mbalimbali wa ofisi za umma.
Katibu alifafanua kuwa nafasi 949 ni kwa ajili ya waajiri walioainishwa
katika ofisi za wizara, halmashauri na nyingine 185 ni za taasisi na
wakala mbalimbali za Serikali.
Aidha, amewataka waombaji wote wa fursa za ajira kufungua matangazo yote
mawili ya kazi na kuzingatia masharti ya Matangazo yote kama yalivyo
katika lugha ya Kiingereza na Kiswahili kabla ya kutuma maombi yao
Aprili 9, 2013.
Daudi alifafanua kuwa waajiri ambao watatoa ajira hizo ni makatibu wakuu
Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Fedha, Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi
na Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya
Maendeleo Jinsia na Watoto, Wizara ya Kazi na Ajira na Ofisa Mtendaji
Mkuu Wakala wa Vipimo.
Wengine ni Makatibu wakuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Kilimo
Chakula na Ushirika, Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Sayansi na
Teknolojia, Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi, Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi, Wizara ya Maji na Katibu Ofisi
ya Rais Maadili.
Wengine ni Makatibu Tawala wa Mikoa ya Kagera, Iringa, Ruvuma, Mbeya,
Mwanza, Shinyanga, Manyara, Dar es Salaam, Morogoro, Geita, Pwani, Mara,
Kilimanjaro, Lindi, Singida, Tabora, Tanga, Katavi na Arusha; pamoja na
wakurugenzi wa halmashauri za majiji na manispaa Mwanza, Iringa,
Songea, Shinyanga, Morogoro, Singida, Kigoma/ Ujiji na Temeke.
Nafasi nyingine ni kwa ajili ya wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya
Mufindi, Kyela, Rungwe, Mbeya, Chunya, Biharamulo, Bukoba, Muleba,
Namtumbo, Songea, Morogoro, Makete, Mkuranga, Mbinga, Tunduru, Ukerewe,
Sengerema, Ilemela, Busega, Maswa na Meatu.
Nyingine ni Wilaya za Shinyanga, Kishapu, Kilosa, Msalala, Rufiji,
Rorya, Ruangwa, Lushoto, Mkinga, Mpanda, Monduli, Ngorongoro, Kigoma,
Nachingwea, Rombo, Same, Singida, Urambo, Tabora, Babati, Mbulu,
Simanjiro na Kiteto.
Pia zimo Wilaya za Handeni, Pangani, Kibondo, Chamwino Mtwara, Nanyumbu,
Mpwapwa, Kongwa na Tandahimba pamoja na halmashauri za miji ya Njombe
na Kibaha. Nafasi nyingine ni za Baraza la Kiswahili la Taifa (Bakita)
na Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa).
Nafasi hizo zilizotangazwa zimegawanyika katika kada zifuatazo;
Mchambuzi Mifumo ya Kompyuta daraja la II – (nafasi 10), Ofisa Vipimo II
– nafasi 6, Mpima Ardhi, daraja la II (nafasi 26), Mhandisi daraja la
II – Ufundi Umeme – Nafasi 9, Ofisa Mipango Miji daraja la II– nafasi 13
na Mhandisi daraja la II - Ujenzi (Nafasi 16).
Pia wanahitajika wahandisi daraja la II - Maji (Nafasi 13), Ofisa Misitu
daraja la II (nafasi 7), Ofisa wa Sheria daraja la II – nafasi 3,
Mtakwimu daraja la II – nafasi 8 na nyingine mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment