Mlezi wa chama cha wakulima wa pamba nchini na msemaji
wa wabunge wanaotoka katika mikoa inayolima zao la pamba nchini,mbunge wa Maswa
Magharibi kupitia Chadema mheshimiwa John Shibuda amewapigia filimbi wasukuma
kwa kuwataka kuamka na kueleza wazi wazi matatizo yanayowakabili badala ya
kukaa kimya na kusema hakuna tatizo(Nduhu Tabhu” wakati kuna tatizo
linawasumbua.
Mheshimiwa Shibuda ameyasema hayo jana mjini Shinyanga
wakati wa kongamano la siku moja la wadau wa pamba mjini Shinyanga lililoandaliwa
na Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania(MVIWATA) na wadau wa pamba kutoka
mikoa ya Mara,Simiyu,Geita na Shinyanga.
Kongamano hilo lililenga kujua na kupata ukweli juu ya
kile kilichotokea kuhusiana na mbegu mpya ya pamba UK91(zenye kipara)
iliyozalishwa na kusambazwa na kampuni ya Quton ambapo mbegu hizo hazikuota
vizuri na kuwaletea hasara kubwa wazalishaji wa pamba.
Mheshimiwa Shibuda alisema ni wakati sasa kabila la
wasukuma ambao ni wakulima wakuu wa zao la pamba kusema matatizo yanayowakabili
hususani katika kilimo cha pamba kwani wamekuwa wakipata hasara na kukaa kimya.
Alisema hapa nchini wasukuma wanafanyiwa dhuluma
kutokana na tabia yao ya ukimya yaani Nduhu Tabhu kwa kila jambo hata kama
linawaumiza.
0 comments:
Post a Comment