TANGAZO KWA UMMA
TANGAZO
JESHI LA KUJENGA TAIFA, LINAKANUSHA TAARIFA ZINAZOSAMBAZWA KWA
KUTUMIA UJUMBE MFUPI WA MANENO (SMS) KATIKA SIMU ZA VIGANJANI NA MTANDAO
WA JAMIIFORUM.COM, KWAMBA VIJANA WA KUJITOLEA NA MUJIBU WA SHERIA
WANAOENDELEA NA MAFUNZO KATIKA MAKAMBI YA JKT WANAKUFA KWA UKATILI,
WAKITOLEA MFANO KAMBI YA JKT OLJORO ARUSHA KWAMBA KUNA VIJANA WATATU
WAMEFARIKI DUNIA.UMMA UFAHAMU KUWA TAARIFA HIZO SI ZA KWELI NI UPOTOSHAJI KWA VIJANA NA WATANZANIA. UKWELI NI KWAMBA KUNA KIJANA MMOJA WA KIKE HONORATA VALLENTINE OISO ALIYEFARIKI KATIKA KIKOSI CHA JKT OLJORO ARUSHA KWA UGONJWA WA UPUNGUFU WA DAMU (ANAEMIA) ULIOSABABISHWA NA MALARIA. SIO VIJANA WATATU KAMA
INAVYOELEZWA KWENYE UJUMBE UNAOSAMBAZWA. WAZAZI WA KIJANA ALIYEFARIKI PIA WALITHIBITISHA KUWA KIJANA WAO ALIKUWA NA MATATIZO YA UPUNGUFU WA DAMU.
JESHI LA KUJENGA TAIFA LINASISITIZA KUWA HAKUNA UKATILI WOWOTE UNAOFANYWA KWA VIJANA WANAOENDELEA NA MAFUNZO KATIKA MAKAMBI YA JKT.
JKT LINALAANI KITENDO HICHO NA LINAFUATILIA ILI KUBAINI CHANZO CHAKE. MTU YEYOTE ATAKAYEBAINIKA KUWA NDIYE CHANZO CHA UJUMBE HUO, HATUA ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA DHIDI YAKE.
JESHI LA KUJENGA TAIFA LINAWAKUMBUSHA VIJANA NA WATANZANIA KUWA MAKINI NA MATUMIZI MABAYA YA SIMU ZA MIKONONI NA MITANDAO YA JAMII, HASA KWA TAARIFA ZINAZOHUSISHA JESHI.
TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA MAKAO MAKUU YA JKT
0 comments:
Post a Comment