
BAADA ya vuta nikuvute ya wazazi wa wanafunzi, Hilary na Hamis ‘watoto wa Diamond’ walioshinda katika shindano la kucheza Ngololo mwaka jana na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuahidi kuwasomesha katika shule ya East Africa International iliyopo Mikocheni, Dar huku akishindwa kuwalipia ada na watoto hao kurudishwa nyumbani, hatimaye wamerejeshwa tena shuleni.

Ilidaiwa kwamba wamewakataza kuzungumza
kwenye vyombo vya habari kutokana na kwamba walichukizwa na habari hiyo
kuvuja na kuripotiwa na gazeti hili kwa mara ya kwanza.

“Wale watoto wamerudi shule tayari baada
ya kukaa nyumbani kwa miezi kadhaa, naamini hata gazeti lenu lilisaidia
sana kuwashtua kwani vinginevyo wasingerudi na ndiyo maana hata wazazi
waliambiwa wasiongee na ninyi,” kilisema chanzo hicho.

Naye mmoja wa wazazi wa watoto hao kwa
sharti la kutokutajwa alisema: “Kwa sasa niko safarini ila ni kweli
watoto wamerudi shule ila mambo bado hayajawa mazuri sana, sema ndiyo
wako kwenye mazungumzo zaidi na suala hilo nimewakabidhi ndugu zangu
ambao wako eneo la tukio ili walishughulikie.”
0 comments:
Post a Comment