Friday 3 July 2015

Wagombea Urais Wanne (4) CCM washindwa kurejesha Fomu Dodoma

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Wagombea 38 kati ya 42 wanaoomba kuteuliwa na CCM kugombea Urais,wamerejesha fomu hadi saa 10:30 jioni julai 2,2015.Kati ya hao Wagombea wanne waeshindwa kurejesha fomu.

Hapa chini ni majina ya wagombea urais ambao wameshindwa kurejesha fomu hizi.

Wagombea ambao hawajarejesha fomu ni pamoja na Dr Kalokola, Hellena Dina Elinawinga, Anthony Chalamila na Peter Nyalali

Baada ya kukamilika kwa kazi ya urejeshaji wa fomu, makada hao 38 watasubiri kufanyika kwa vikao vya juu vya maamuzi.

Vikao hivyo ni pamoja na Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa itakayokutana Julai 7 na Kamati Kuu (CC) itakayokutana Julai 8, chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete, ikifuatiwa na kikao cha Nec Julai 9, mwaka huu.

Mchakato wa kumpata mgombea urais atakayepeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, utahitimishwa Julai 11, mwaka huu na Mkutano Mkuu wa Taifa CCM ambao ni maalum kwa ajili kulipigia kura jina la mgombea mmoja kati ya watatu.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger