Ramadhani Singano 'Messi'.
SHIRIKISHO la
Soka Tanzania (TFF), leo limeamua kuwa, mchezaji Ramadhani Yahya
Singano 'Messi' ni huru na sasa anaweza kujiunga na timu yoyote.
Taarifa
kutoka kwenye kikao cha Kamati ya Sheria Maadili na Hadhi za Wachezaji
ya TFF kilichofanyika leo, imesema kwamba Simba SC walishindwa
kutekeleza baadhi ya vipengele vya Mkataba, hivyo wanapoteza haki za
kummiliki mchezaji huyo.
Chini
ya Mwenyekiti wake, Richard Sinamtwa, Kamati hiyo imejiridhisha Messi
hakuwahi kupewa nyuma ya kuishi na Simba SC jambo ambalo ni kinyume cha
Mkataba baina yake na klabu hiyo.
Simba
SC iliwakilishwa na Mwenyekiti wake wa Kamati yake ya Usajili, Zacharia
Hans Poppe na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Collins Frisch wakati Messi
alifika na Mwenyekiti wa Chama cha Wachezaji Tanzania (SPUTANZA), Mussa
Kisoky..
Maamuzi
haya ni faraja kwa Messi ambaye anahusishwa kwa kiasi kikubwa na
kuhamia Azam FC. Messi aliyeibukia timu ya vijana ya Simba SC miaka
minne iliyopita, hivi karibuni ameibua shutuma dhidi ya klabu yake hiyo
kwamba imeghushi Mkataba wake. Messi anadai Mkataba wake halali ulikuwa
unamalizika mwaka huu, na si huu wa sasa ambao inaelezwa utamalizika
mwakani.
Lakini
Simba SC imeendelea kusistiza mchezaji huyo alikuwa ana Mkataba wa
miaka mitatu. Awali, Sekretarieti ya TFF, chini ya Katibu wake,
Selestine Mwesigwa ilizikutanisha pande zote mbili, mchezaji na Simba SC
na kuamuru waketi chini na kutayarisha Mkataba mpya baada ya kuona huu
wa sasa una mushkeli. Hata hivyo, Messi akakataa na kuamua kulihamishaia
suala hilo Kamati ya Sheria ambayo leo imempa kile alichotaka ‘kuwa
mchezaji huru’.
Safari FIFA?; Hans Poppe amesema kwamba watakwenda mbele kusaka haki zao
Mwenyekiti
wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Hans Poppe amesema kuwa, baada ya
matokeo hayo, wanakwenda kukutana ili kujua hatua zaidi za kuchukua,
lakini dhahiri hawataishia hapo.
“Tuliwasilisha
ushahidi wote mbele ya Kamati, tumeonyesha mshahara wake ulikuwa kiasi
gani na tumeonyesha kwa nini alikuwa anapewa laki moja (100,000) zaidi.
Ili
akalipie kodi ya nyumba, lakini bado hatukueleweka. Tunaamini hapa si
mwisho, vipo vyombo vingine ambavyo vitatupa haki yetu, tunakwenda
kukutana kuangalia uwezekano wa kulipeleka suala hili huko,”amesema
Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
SHARE
0 comments:
Post a Comment