Mbunge wa Mpanda Mjini Mhe. Said Arfi akizungumza na waandishi wa habari. Picha ya maktaba. |
Akizungumza
mjini Mpanda katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa
Shule ya Msingi Kashaulili, jana Mhe Saidi Arfi aliwaeleza wananchi wa
Mpanda kuwa uanachama wake ndani ya CHADEMA utakoma mara tu baada ya
kuvunjwa Bunge Julai 9.
Pia, alitumia mkutano huu kuwaaga wananchi wa jimbo hilo akisema hatagombea tena nafasi hiyo aliyoitumikia kwa miaka kumi.
Mhe.
Arfi alifafanua kuwa hayuko tayari kugombea jimbo hilo kupitia chama
chochote cha siasa na kauli hiyo imelenga kuondoa uvumi uliokuwa umeenea
kwamba alikuwa na nia ya kugombea kupia ama ACT – Wazalendo au CCM.
Alisema
amekuwa akishangazwa na kauli ambazo zimekuwa zikitolewa na baadhi ya
wanachana na wapenzi wa CHADEMA kuwa hajafanya lolote kwenye chama
hicho. Alisema kama kuna mtu anayekifahamu vizuri chama hicho ni yeye,
hivyo haoni sababu za watu kumbeza. Alisema alikuwa ameamua kukaa kimya
na kuwa akiamua ‘atamwaga mboga’ ili watu wafahamu upungufu ulioko ndani
ya chama hicho.
Alisema hagombei katika jimbo hilo na kama kweli chama hicho kina nguvu, basi kilitetee, akisisitiza kuwa ana uhakika jimbo hilo litakwenda CCM kwa kuwa wananchi wa Mpanda Mjini walikuwa na mapenzi na mtu siyo chama
0 comments:
Post a Comment