Naibu waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dokta Marry Mwanjelwa amezitaka taasisi za umma kuhakikisha suala la usalama wa taarifa za serikali linakuwa la lazima wakati wa kubuni,kusanifu,kujenga,kusimika na kuendesha mifumo ya TEHAMA. Dokta Mwanjelwa alitoa agizo hilo jiji Dodoma wakati akifungua kikao kazi cha pili cha serikali mtandao. Amesema njia moja wapo ya kujihakikishia usalama ni kuhakikisha utengenezaji wa mifumo unazingatia programu ambazo wataalamu wao wanaweza kutambua kinachofanyika badala ya kuwa na mifumo ambayo hawajui kinachofanyika nyuma ya pazi. “kwa namna ya kipekee kabisa…
0 comments:
Post a Comment