Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amefika nyumbani kwa familia ya Ruge Mutahaba na kutoa pole za msiba ambapo pia ameweza kumwelezea marehemu Ruge kama mtu mwenye uthubutu kwa jamii.
Dk. Kigwangalla ameweza kuonana na kutoa pole kwa wafiwa ndugu,jamaa na marafiki akiwemo Baba mzazi Mzee Mutahaba pamoja Mama wa Ruge Bi. Cristina Mutahaba na kutoa pole zake hizo pamoja na rambirambi alizokabidhi kwa Mama mzazi.
Dk. Kigwangalla amemuelezea marehemu kama mtu wa kuigwa kwani alijituma katika kuhakikisha anatimiza malengo yake aliyopangiwa ama kujipangia.
"Ruge alikuwa mtu wa watu na alisimama katika mipango sahihi hata nikamchagua kwenye Kamati za kuendeleza masuala ya Utalii ikiwemo ile ya Tanzania Unforgettable." alieleza Dk Kigwangalla.
Aidha, Dk Kigwangalla ameweza kuungana na viongozi wengine pamoja na ndugu na jamaa.
Awali taaifa ya Msemaji wa Familia Bw. Anic Kashasha amesema kama mipango itakwenda kama ilivyopangwa mwili wa marehemu Ruge Mutahaba utawasili Ijumaa na utaagwa rasmi siku ya Jumamosi jijini Dar es salaam, Baada ya kuagwa utasafirishwa kwenda Bukoba siku ya jumapili na kuzikwa siku ya jumatatu huko Bukoba mkoani Kagera.
Na Andrew Chale - Dar es salaam
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamisi Andrea Kigwangalla akitoa pole kwa Mama mzazi wa Ruge Mutahaba alipoenda kutoa pole mapema leo Februari 27.2019.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamisi Andrea Kigwangalla akiteta jambo na Mbunge pole wa Kigoma Zitto Kabwe katika msiba wa Ruge Mutahaba alipoenda kutoa pole mapema leo Februari 27.2019.
0 comments:
Post a Comment