Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani nchini, kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi, Fortunatus Muslim ameagiza dereva wa gari lililosababisha ajali iliyoua watu 19 akiwamo yeye mwenyewe katika Mlima Senjele wilayani Mbozi mkoa wa Songwe ashtakiwe.
Aidha, ametoa maagizo matatu ya kutekelezwa haraka ili kukomesha ajali zinazojitokeza mara kwa mara na kuua watu wengi katika eneo hilo.
Alitoa maagizo hayo jana siku moja baada ya kutokea ajali ya lori kugongana na basi aina ya Coaster na kusababisha vifo vya watu 19 katika mlima Senjele Mbozi mkoa wa Songwe.
Akizungumza katika eneo ajali hiyo iliyotokea Februari 21 mwaka huu saa 3:15 usiku, kamanda Muslim alitaja jambo la kwanza ni polisi kufanya uchunguzi wa kina ili kupata chanzo cha ajali hiyo na hatua kuchukuliwa kwa dereva na mmiliki wa gari hilo.
“Hata kama dereva wa gari hilo amefariki lakini ipo sheria inayotumika kumshitaki na pia mmiliki wa lori hilo amekwishajulikana na askari wa usalama barabarani wanamfuatilia ili naye aje ajibu tuhuma za kuruhusu gari lake kutembea barabarani likiwa bovu,” alisema.
Na Stephano Simbeye, Mwananchi
0 comments:
Post a Comment