Monday, 25 February 2019

NDOO 226 ZENYE SAMPULI ZA MIAMBA YA MADINI 883 ZAKAMATWA MWANZA

...

Kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Mwanza inalishikilia gari lori aina Fuso lililokuwa likisafirisha shehena ya sampuli za madini kutoka mkoani Geita kwenda jijini humo.

Mwenyekiti wa kamati hiyo mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella jana alisema gari hilo lilikamatwa jana na ndoo 226 zenye sampuli za miamba ya madini 883 mali ya Mgodi wa Dhahabu Geita (GGM).

“Gari hilo lilikamatwa na askari waliokuwa doria baada ya kubaini wahusika walikuwa na upungufu wa vibali vinavyoruhusu kusafirisha mzigo huo kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine,” alisema.

Mongella alisema shehena hiyo ilikuwa ikisafirishwa kwenda kwenye maabara ya kupima madini hayo ya SGS iliyopo jijini Mwanza.

Kutokana na hali hiyo, mkuu huyo wa mkoa aliagiza kuchunguzwa na kufuatilia uhalali wa sampuli hizo huku akiwataka watendaji wa Serikali kufanya kazi kwa uadilifu.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger