Mipango ya kuurejesha nchini mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba, imekamilika Afrika Kusini na mwili wake unatarajiwa kuwasili kesho majira ya saa 8:00 mchana katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Msemaji wa familia Bw. Annick Kashaha amesema kuwa mara baada ya kuwasili mwili wa Ruge hapo kesho utapokelewa na kupelekwa katika hospitali ya Lugalo Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuhifadhiwa hadi Jumamosi.
Amesema kuwa mwili wa Ruge ambaye pia alikuwa moja ya muasisi wa Clouds Media Group, utaagwa Jumamosi majira ya saa tano katika eneo la Karimjee, ambapo wakazi wa Dar es Salaam watapata fursa ya kutoa heshima zao za mwisho.
Mwili wa Ruge aliyefariki dunia nchini Afrika Kusini juzi wakati akipatiwa matibabu ya figo utawasili mjini Bukoba kwa ndege Jumapili na maziko yake yatafanyika siku ya Jumatatu Kizuku Bukoba.
0 comments:
Post a Comment