Kushoto ni Hans van der Pluijm na Mwinyi Zahera
Klabu ya soka ya Azam FC, imewafuta kazi makocha wake, mkuu Hans van der Pluijm na msaidizi wake Juma Mwambusi kutokana na mwenendo mbovu wa timu katika michezo ya hivi karibuni kwenye ligi kuu.
Hans ambaye alikuwa kwenye msimu wake wa kwanza ndani ya timu, amekuwa hapati matokeo mazuri katika mechi kadhaa za ligi ambapo katika michezo mitano amembulia alama 3 pekee kati ya 15.
Matokeo ya Azam mechi 5 za mwisho.
Azam 1-3 Simba
Coastal 1-1 Azam
Prisons 1-0 Azam
Lipuli 1-1 Azam
Azam 1-1 Alliance
Hata hivyo Azam FC ambayo imecheza mechi 25 za ligi haikuwa kwenye nafasi mbaya ambapo ikiwa na alama 50 ipo katika nafasi ya pili nyuma ya Yanga wenye alama 61 na mbele ya Simba wenye pointi 45.
Kocha anayechukua mikoba yao.
Kutoka katika chanzo cha karibu na kocha wa Yanga Mwinyi Zahera, inaelezwa kuwa tayari kocha huyo yupo kwenye mazungumzo na Azam FC na wamefikia pazuri hivyo muda wowote kuanzia kesho atatangazwa kuwa kocha wa Azam FC.
0 comments:
Post a Comment