Meneja Miradi wa shirika la Young Women Leadership (YWL),Veronica akizungumza wakati wa mafunzo kwa walimu wa Manispaa ya Shinyanga kuhusu afya ya uzazi kwa vijana na ukatili wa kijinsia -Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog
***
Shirika la Young Women Leadership (YWL) limetoa mafunzo kwa walimu kutoka shule tisa za sekondari na msingi za Manispaa ya Shinyanga kuhusu afya ya uzazi kwa vijana na ukatili wa kijinsia kwa lengo la kuimarisha masuala ya usawa wa kijinsia na huduma za afya uzazi kwa wanafunzi.
Mafunzo hayo ya siku mbili yaliyoanza Februari 26 hadi 27,2019 yamefanyika katika ukumbi wa Simej Hoteli Mjini Shinyanga na
kukutanisha walimu 40 kutoka shule za sekondari Kizumbi,Mwawaza,Old Shinyanga,Town,Ibinzamata na shule za msingi Mwantini,Bugayambelele,Mwadui na Azimio.
Meneja Miradi wa shirika la YWL linalojihusisha na masuala ya uongozi kwa mabinti,kutokomeza mimba na ndoa za utotoni na kuimarisha uchumi kwa kaya, Veronica Massawe alisema mafunzo hayo ni muhimu kwa ustawi wa wanafunzi shuleni na jamii kwa ujumla.
“Walimu wanakaa muda mwingi na watoto shuleni kuliko wazazi nyumbani,mafunzo haya yatasaidia kuimarisha usalama na afya za watoto wawapo shuleni na hata kwenye jamii”,alieleza.
“Walimu hawa tuliowajengea uwezo katika masuala ya usawa wa kijinsia na huduma za afya ya uzazi wanatoka kwenye shule zenye wanafunzi tuliowalenga kuwafikia na wanapatiwa elimu hii, wanafunzi hao wengi wao wanatoka kwa wazazi na walezi wao ambao tunawapatia stadi za malezi na makuzi bora ya watoto na kuimarisha uchumi wa familia”,alifafanua Massawe.
Alisema YWL inatekeleza mradi wa Kutokomeza Mimba na Ndoa za Utotoni ulioanza Januari 2019 na utamalizika mwezi Desemba mwaka huu ukiwa na lengo la kuwafikia walimu,wazazi, wanafunzi na wahanga wa ndoa za utotoni ili kuwapa elimu kuhusu masuala ya afya ya uzazi,stadi za malezi na makuzi bora ya watoto na kuimarisha uchumi wa familia.
Nao washiriki wa mafunzo hayo waliwaomba viongozi wa serikali kutumia mikutano ya kuwaelimisha wananchi kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia huku walilishauri ngoma na jeshi la sungusungu vitumike kukusanya watu ili wapewe elimu hiyo.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Meneja Miradi wa shirika la Young Women Leadership (YWL),Veronica Massawe akizungumza wakati wa mafunzo kwa walimu wa Manispaa ya Shinyanga kuhusu afya ya uzazi kwa vijana na ukatili wa kijinsia katika kumbi wa Simej Hoteli Mjini Shinyanga -Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Meneja Miradi wa shirika la Young Women Leadership (YWL),Veronica Massawe akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Walimu wakiwa ukumbini.
Mafunzo yanaendelea.
Afisa Ustawi wa Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Agnes Ginethon akitoa mada kuhusu Mpango Mkakati wa Kupinga Ukatili kwa wanawake na watoto (MTAKUWWA).
Kulia ni Afisa Ustawi wa Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Agnes Ginethon akieleza kuhusu sababu zinazochangia ukatili wa kijinsia kuwa ni umaskini,mila na desturi,ulevi kupindukia na madawa ya kulevya pamoja na mmomonyoko wa maadili katika jamii.
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada ukumbini.
Mwalimu Jovini Bartholomew kutoka shule ya sekondari Ibinzamata akichangia hoja kuhusu masuala ya afya ya uzazi.
Mwalimu Grace John Bunga kutoka shule ya msingi Azimio akichangia hoja wakati wa mada kuhusu afya ya uzazi.
Mwalimu Dismas Humay kutoka shule ya msingi Bugayambelele akichangia hoja wakati wa mafunzo hayo.
Mwalimu Neema Mcharo kutoka shule ya sekondari Town akizungumza wakati wa mafunzo hayo na kuwahamasisha walimu kuwa na muda wa kuwajenga kusaikolojia wanafunzi.
Mwalimu Robert Mlela kutoka shule ya msingi Mwadui akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Picha ya pamoja washiriki wa mafunzo hayo.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
0 comments:
Post a Comment