Mwanaharakati mmoja Rubaramira Ruranga mwenye umri wa miaka 71 kutoka Uganda na ambaye ni baba wa watoto 11 ameamua kupanga uzazi kupitia njia ya upasuaji ili kuzuia kuzaa watoto wengine.
Ruranga aliwataka wanandoa wachanga kupanga vema uzazi na kujadili idadi ya watoto wanaotaka kupata kabla ya kupitwa na wakati.
Babu huyo alisema anajutia kuwa na mtoto wa miaka 2 kwa sasa kwani ingekuwa vema kwa angekuwa akiwalee wajukuu kulingana na umri wake.
"Niliamua kupanga uzazi kupitia njia ya upasuaji ili nisiwe nikimtatiza mke wangu kila mara eti apange uzazi, yuko na miaka 41 na mimi niko na miaka 71, ningependa wanandoa kupanga uzazi kwa njia ifaayo na wajadiliane ni watoto wangapi wanaotaka kupata kulingana na uwezo wao wa kifedha, msizae watoto hadi uzeeni ambapo badala ya kulea wajukuu eti bado mnalea watoto wenu kama mimi hapa," Ruranga alisema.
Ruranga alisisitiza kuwa upangaji uzazi kupitia njia ya upasuaji yaani vasectomy ni bora zaidi na wanaume wengi kutoka nchi za Afrika Kusini na Nambia wamekumbatia njia hii.
Hata hivyo, utafiti unaonyesha kuwa asilimia 0.1% peke ya Wakenya wamepanga uzazi kupitia njia hii.
0 comments:
Post a Comment