Thursday, 28 February 2019

FISI WANAOTAFUNA NYETI WAZUA GUMZO

...


Uchungu wa kufinywa nyeti ni wa ajabu zaidi kwa wanyama na hata binadamu na hivyo kwa kutaja tu kisa cha aina hiyo, mwili husisimuka. 


Katika Mbuga ya Kitaifa ya Aberdare, nyati dume wanaishi kwa uoga mkubwa sana baada ya fisi katika mbuga hiyo kugeuka katili na kuanza kufanya sehemu hizo muhimu kwa wanayama hao kuwa mlo.

Kulingana na ripoti ya K24 TV, Shirika la Huduma ya Wanyama Pori nchini (KWS) limeanza kuchunguza visa hivyo ili kuokoa nyeti za nyati dume katika Aberdare. 

Shirika hilo sasa linachunguza kuhusu tabia ya fisi ya kuwatesa nyati kwa kunyofoa nyeti zao hali inayoweza kuhatarisha uwepo wa nyati.

 Uchunguzi uliotolewa awali umeonyesha kuwa, sababu ya fisi kufanya hivyo ni kukosekana kwa simba, chui na hata duma ambao kawaida huwaua wanyama wengine na kula nyama kisha kuachia fisi mabaki.

 "Katika hifadhi zingine kuliko na simba, fisi hula mabaki lakini katika Aberdare kunakokosekana simba, wanalazimika kuwinda na katika hali hiyo hawawaui walengwa wao lakini huishia kunyofoa sehemu za miili yao," Lilian Ajuoga, afisa mkuu katika KWS Aberdare alisema.

 "Wakiwinda nyati wadogo na nyeti zao kunyofolewa, basi nyati hao hukua bila ya ishara za kuonyesha wao ni dume," aliongezea. 

Katika hali ya kujilinda, nyati katika mbuga hiyo sasa wameanza kutembeaakundi lakini kwa upande mwingine, fisi nao wameanza kujiweka katika makundi ili kuimarisha uwezo wao wa kufanikiwa katika kuwinda. 

 Hapa itakuwa ni mwenye nguvu mpishe. 


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger