Polisi nchini Kenya wamewakamata watu saba wanaodaiwa kushirikiana kuigiza sauti ya rais Uhuru Kenyatta na maafisa wengine wa serikali katika kumuibia pesa nyingi mfanyabiashara tajiri nchini humo -Naushad Merali.
Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Mmoja wa watu hao alimpigia simu Bwana Merali, ambaye ni Mwenyekiti wa Sameer Africa, aliigiiza sauti ya rais Uhuru kenyatta akimshawishi ampatie pesa za kusaidia mipango ya biashara.
Fedha kamili zilizoibiwa bado hazijafahamika wazi huku vyombo vya habari nchini Kenya vikitofautiana kwamba ni shilingi milioni 10, huku gazeti lingine likiandika kwamba ni shilingi milioni 80.
“kutokana na ugumu wa uchunguzi na idadi ya washukiwa wanaohusika , wakiwemo wale ambao bado hawajapatikana , uchunguzi unatarajiwa kujumuisha nyaraka nyingi zikiwemo zile za benki pamoja na uchunguzi wa kina wa data za mawasiliano ya simu”, ilieleza ripoti ya polisi iliyonukuliwa na gazeti la Daily Nation.
Wakati wa operesheni hiyo, polisi walikamata magari aina ya Toyota Land Cruiser, Toyota Mark X , Toyota Axio na Toyota Crown.
Uchunguzi huo unatarajiwa kubaini ikiwa magari hayo yana uhusiano na uhalifu huo.
Mpaka sasa Bwana Merali (aliyetapeliwa) na rais Kenyatta bado hawajazungumzia juu ya tukio la kukamatwa kwa watu hao.
0 comments:
Post a Comment