Chama Cha Wananchi (CUF) upande wa katibu mkuu Maalim Seif Sharif Hamad kimemuomba Jaji Mkuu na Jaji kiongozi kusaidia kusomwa hukumu katika shauri linalohusu uhalali wa uenyekiti wa Profesa Ibrahim Lipumba. Wito huo umetolewa leo jijini Dar es salaam na Mnadhimu wa Kambi ya CUF Bungeni ambaye pia ni mbunge wa Malindi Ally Saleh wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema shauri hilo lililopo mbele ya Jaji Dr.Benhajj Massoud tayari limeshasikilizwa kwa pande zote mbili na lipo katika hatua ya kutolewa hukumu. Mnadhimu huyo amesema kuwa kucheleweshwa kutolewa kwa hukumu hiyo kumeathiri…
0 comments:
Post a Comment