Mbunge wa Kawe (Chadema), Halime Mdee anaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi baada ya kuhojiwa na kunyimwa dhamana.
Wakili wake, Hekima Mwasipu alisema Mdee ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema, amehojiwa kwa muda wa saa mbili na kunyimwa dhamana.
Amesema Mdee alipokea wito na mkuu wa upelelezi mkoa wa kipolisi Kinondoni (RCO) leo kufika kituoni hapo kwa ajili ya mahojiano kutokana na kauli ya uchochezi aliyoitoa kwenye mkutano kata ya Mikocheni Februari 21.
"Polisi wamemhoji kwa masaa mawili kutokana na kauli aliyoitoa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Mikocheni," amesema wakili Hekima.
Mdee ambaye alifika kituoni hapo saa tatu asubuhi alianza kuhojiwa saa 6:15 hadi saa 8:20 ambapo baada ya mahojiano hayo alinyimwa dhamana.
0 comments:
Post a Comment