Watu wanaopenda kufanya ngono na wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari nchini sasa kukamatwa.
Kazi ya kuanza kukabiliana na watu wenye tabia hiyo inaanzia mkoani Kilimanjaro ambapo Kasim Majaliwa, Waziri Mkuu ameagiza waliowapa mimba wanafunzi mkoani humo wakamatwe.
Ni baada ya taarifa ya mkoa huo kuonesha kwamba, kuanzia Januari hadi Desemba mwaka 2018, jumla ya wanafunzi wa kike 57 walipachikwa mimba na hatimaye kukatisha masomo yao.
Taarifa hiyo ilimshtua Waziri Majaliwa na hasa baada ya kuelezwa kuwa, katika kesi hizo 57 za wanafunzi kupachikwa mimba, ni kesi sita tu ndio zilizofikishwa mahakamani.
Agizo hilo la kukamatwa malevi hao wa ngono wote limetolewa na Waziri Majaliwa mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano uliofanyika katika Uwanja wa Isanja, Sanya Juu katika Wilaya ya Siha, Kilimanjaro.
Chanzo- Mwanahalisionline
0 comments:
Post a Comment