Picha haihusiani na habari hapa chini
Mwanafunzi mmoja wa darasa la saba katika shule ya msingi ya Mikuyuni eneo la Kibwezi kaunti ya Makueni nchini Kenya kufariki dunia baada ya kupigwa na mwalimu.
Akidhibitisha kisa hicho, kamanda mkuu wa polisi kata ndogo ya Kibwezi Ben Chagulo alisema mwanafunzi huyo alikimbizwa katika hospitali ya AMREF lakini alifariki dunia kabla ya kuhudumiwa na madaktari.
Kulingana na ripoti ya maafisa wa polisi mvulana huyo alifariki baada ya kuchapwa vibaya na mwalimu huyo.
Mamaake mwathiriwa Josephine Ndunge amesema kuwa alipokea habari za kifo cha mwanawe kupitia kwa mwalimu mmoja aliyempigia simu.
"Nilipigwa simu na mmoja wa walimu aliyeniambia kuwa kijana wangu hajihisi vema baada kuadhibiwa na mwalimu. Nilifululiza hadi shuleni humo ambapo nilimpata mwanangu akivunja damu kwa wingi," Mamake marehemu alisema.
Aidha, Chagulo alisema tayari uchunguzi umeanzishwa kufuatia kisa hicho na atatoa taarifa kamili.
Mwalimu huyo aliyetambulikana kwa majina kama Stanley Kithyaka alikamatwa baada ya kutorokea mafichoni kwa saa chache na anashikiliwa katika kituo cha polisi cha kibwezi.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi wafu cha hospitali ya Makindu ukisubiri kufanyiwa upasuaji kubaini chanzo cha kifo chake.
0 comments:
Post a Comment