Na Amiri kilagalila Mkuu wa mkoa wa Njombe CHRISTOPHER OLESENDEKA amewaagiza viongozi wa serikali za mitaa wakiwemo wenyeviti wa vijiji kuhakikisha wanashiriki katika zoezi la kutoa taarifa za wahusika wa mauaji mkoani Njombe huku akiapa kuanza kushughulika na viongozi hao wa vijiji endapo yatatokea mauaji yanayofanana na yaliyotokea mkoani humo. OLESENDEKA alitoa maagizo hayo hii leo katika viwanja vya polisi mjini makambako wakati akizungumza na mamia ya wananchi wa mji huo kwa lengo la kuwaomba wananchi kuonyesha ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama katika kushiriki kuwafichua wanaohusika katika mauaji…
0 comments:
Post a Comment