Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini Richard Kasesela
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini Richard Kasesela amelishauri Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT Dayosisi ya Iringa kumuondoa /kutomfumbia macho aliyekuwa Msaidizi wa Askofu wa Dayosisi hiyo mchungaji Yusto Kinyori kwa tuhuma ya kufanya mapenzi na mtoto wa mchungaji mwenzake kwenye gari.
Kasesela amesema hayo kwenye Mkutano Mkuu wa kumchagua Msaidizi wa Askofu wa kanisa hilo uliofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT usharika wa Ipogolo ambapo amesema kuwa anayo video clip ikionesha mchungaji huyo akifanya mapenzi kwenye gari na mtoto wa mchungaji mwenzake.
Kasesela amesema kuwa kinachomuuma zaidi viongozi wa dini ndiyo wanaotumwa kwenda serikali kuwawakilisha baadhi ya viongozi au kutoa matamko mbalimbali kwa niaba ya kanisa lakini kiongozi huyo amekengeuka kwa sababu ya kitendo alichokifanya na kushauri kanisa limuondoe haraka kwa sababu analiaibisha kanisa.
Kwa upande wake Askofu wa Kanisa hilo Dayosisi ya Iringa Mchungaji Blastone Gavile amesema mkutano huo maalumu umefanyika kutokana na vikao vilivyofanyika mwishoni mwa mwakajana kujadili ofisi ya msaidizi wa askofu kutokana na tuhuma zilizokuwa zikimkabili.
Mara baada ya kufanya uchaguzi huo walimpata msaidizi wa askofu Askari Mgeyekwa ambaye alikuwa mkuu wa KKKT usharika wa Kihesa na ameibuka kidedea kwa kupata kura 480, kura za hapana 17 na zilizoharibika 10 na jumla ya wapiga kura walikuwa 457.
Chanzo - EATV
0 comments:
Post a Comment