Watu
14 akiwemo Mchina, wanahofiwa kufa baada ya kufukiwa katika mgodi wa
dhahabu wa Kampuni ya RZ Union Mining Ltd uliopo Kata ya Nyarugusu
mkoani Geita.
Mkuu
wa Mkoa wa Geita, Ezekiel Kyunga jana alisema watu hao wamefukiwa chini
ya mgodi baada ya mlango wa kuingilia kwenye shimo la mgodi kumeguka
udongo na kujiziba.
“Usiku
wa kuamkia leo (jana) saa tisa kwenye mgodi huo unaoendeshwa na
Wachina, mlango wa kuingilia mgodini mmoja ulimeguka na kujifunga watu
14 wakiwa ndani,” alisema Kyunga.
Kyunga alisema kwa mujibu wa kitabu cha orodha ya watu wanaojiandikisha kuingia mgodini, kuna majina ya Watanzania 12 na Mchina.
Aidha,
alisema mbali na watu hao 13, pia kuna Mtanzania mmoja ambaye aliingia
bila kujiandikisha na hiyo ni kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio
hilo hivyo kufanya idadi ya watu waliofukiwa kuwa 14.
Kyunga
alisema tangu jana asubuhi jitihada mbalimbali za kuondoa udongo
kuwaokoa watu hao zinaendelea wakitumia mitambo na wataalamu.
“Kwa
kusaidiana na Kampuni ya Geita Gold Mine (GGM) na wataalamu wengine,
jitihada zinaendelea ili kuhakikisha tunawaokoa watu hao,” alisema Kyunga.
Alisema
wakati huo huo wamefanikiwa kutoboa eneo jingine na kupitisha mabomba
ya hewa ya oksijeni ili kuwafanya watu hao wasikose hewa.
0 comments:
Post a Comment